Featured Posts
Jumatatu, 2 Oktoba 2017
Alhamisi, 26 Juni 2014
WALIMU WA SHULE ZA MSINGI IRINGA MJINI WAFANYA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI
Baadhi ya walimu wa shule za msingi Iringa mjini wamehudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na Taasisi ya Decision Foundation. Walimu hao wamejifunza namna ya kuanzisha na kusimamia biashara, faida za utandawazi katika biashara na harakati za ukombozi wa Taifa la Tanzania. Walimu hao wameazimia kuanzisha umoja wa kibiashara ili waweze kujikomboa ki-uchumi.
Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyotolewa na Decision Foundation Iringa tarehe 25/26/2014 |
Walimu wakifuatilia mafunzo kwa ya ujasiriamali kwa umakini |
Mwl. Meela, Sugara na Annet Ulaya wakifuatilia mafunzo kwa furaha |
Ijumaa, 20 Juni 2014
TAMU ZENYE CHUNGU KATIKA UCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU TANZANIA
HAKIKA KUNA TAMU ZENYE CHUNGU NA CHUNGU ZENYE SALAMA KWA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU TANZANIA
Sheria
za madini nchini pamoja na mambo mengine, haziruhusu mtu kushika, kukutwa au
kufanya biashara ya madini yoyote bila ya kuwa na leseni. Sheria hiyo
inamruhusu mwekezaji yeyote wa ndani na nchinya nchi, kuomba leseni ya
uchimbaji sehemu yeyote kwa mujibu wa sheria na kutoa fidia kwa mali zilizopo
juu ya ardhi kwa wote watakaokuwepo katika eneo lililoombewa kibali. Ndiyo
maana baadhi ya watanzania hawaielewi vizuri sheria hii itakayoelezewa vizuri
hapo chini. Utaratibu huu wa kuchimba dhahabu kienyeji na kuiuza kienyeji
ulimkumba mchimbani mmoja huko Nyalugusu, Mkoa wa Geita ambaye alifanikiwa
kupata madebe matatu yaliyojaa dhahabu na kukataa fedha badala yake aliwaomba
wanunuzi eti wampatie treni {gari moshi}.
Mzee
huyo aliyejitamblisha kwa jina la mangida, alisema yeye shida yake ilikuwa
apewe treni aimiliki kwani aliipenda sana. Watu walio karibu nae walimwambia
mwandishi wa habari hizi kuwa, wanunuzi hawakumwelewa muuzaji huyo na waliamua
kumuacha hotelini mwanza na kuelekea huko India. Tukio hili ni la muda mrefu,
takribani miaka 40 iliyopita. Picha chini ni Muuzaji huyo wa dhahabu akiwa na
mwandishi wa makala hayo bwana Dominick Haule.
Kisheria,
mzee huyu angeliweza kukamatwa na kushtakiwa kwa kisa la kukutwa na madini bila
ya kuwa na leseni wala kibali. Huenda angelikuwa mchimbaji mwenye leseni,
maafisa wa madini wangelimsaidia kuuza madini hayo.
Sheri
za madini zina watatanisha sana baadhi ya watanzania hususani wale wenye
mashamba yaliyopo maeneo yenye madini. Ukiwa na shamba na hata kama una hati ya
kumiliki shamba hilo, sheria inaruhusu utoaji wa leseni shambani kwako ili
mwekezaji anayetafuta mali iliyopo chini ya ardhi, aweze kuipata mali hiyo kwa
sharti ya kukulipa fidia ya kilichopo juu ya ardhi kwani ardhi ni mali ya
serikali. Ni vizuri watanzania wakachukua hatua ya kuzifahamu baadhiya sheria
za madini ili waweze nao kuomba leseni za madini kama watahitaji kufanya hivyo
badala ya kuishia kulia na kulalamika sana kitu ambacho hakitamsaidia mtanzania
wala Taifa kwa ujumla.
Kwa
taarifa zaidi, maoni au maswali wasiliana na dominickhaule@gmail.com
Simu:
0767 11 1173.
Bwana Dominick FN Haule {katikati} akimhurumia mzee Mangida {kulia kwake} kwa kupoteza madebe matatu ya dhahabu |
Mwandishi wa Makala haya {katikati} akizungumza na mzee Mangida {aliyekaa kushoto} ambae alikataa fedha ili auze dhababu madebe 3 kwa kupewa Trani {Gari moshi} |
MAJANGA NA MARAHA YA WACHIMBAJI WADOGO TANZANIA
Mwandishi
wa makala haya amebahatika kupata baadhi ya taarifa nyingi za uchimbaji na
wachimbaji wadogo ambao baadhi yao huamini kuwa kuna sehemu ya ushirikina
inatumika jambo ambalo wataalam wanalipinga vikali. Wachimbaji wadogo wa
dhahabu ambao nchini idadi yao inakaribia milioni tatu 3,000,000 wamekuwa na
changamoto kubwa tatu: -
i.
Tatizo la Kujaa maji migodi yao (mashapo au
shafts}
ii.
Tatizo la Mwamba mgumu wanaoukabili ndani ya
mgodi na jinsi ya kuutoa baada ya kuuvuja
iii.
Tatizo la mtaji
Wakati
utatuzi wa tatizo au changamoto ya kwanza ni kuitatua kwa kupata pampu za maji
zenye uwezo wa kutoa maji haraka wakati uchimbaji unaendelea, tatizo la pili la
mwamba linatatuliwa na mashine za kisasa za kupasulia miamba {jack hammers na
compressors} ambavyo vyote vinahitaji uwekezaji mkubwa kuzidi uwezo wao. Tatizo
la kutoa mwamba au vipande vya mawe na udongo wenye dhahabu linatatuliwa kwa
kupata mshine ya kunyanyulia mizigo aina ya {crane} zinye uwezo wa tani moja na
kuendelea kwani kwa kutumia ndoo, inawachukua matumizi ya nguvu nyingi na muda
mrefu sana. Mashine zingeliwawezesha kutoa kiasi kikubwa cha udongo na mawe kwa
muda mfupi na kufanya kazi ya kusaga kwa muda mrafu wakiwa namali ghafi nyingi
katika stoo zao.
Kuna
faida kubwa pia katika uchimbaji mdogo licha ya kuwa na changamoto mbali mbali
kwani kwa mchimbaji aliyejipanga anakuwa na uwezo wa kuzalisha hadi kilo moja
kila siku. Mwandishi wa makala haya alitembelea mgodi mmoja wa mchimbaji mdogo
ambaye uwezo wake ulikuwani nusu kilo ya dhababu kwa siku. Uwekezaji unaweza
kutumia kiasi cha shilingi milioni mia tatu 300,000,000/= kwa wachimbaji wadogo
wenye uwezo na wanaofuata utaalamu kwani maafisa madini wana taaluma nzuri ya
kushauri masuala ya uchimbaji na kumuwezesha mchimbaji mdogo kufikia uwezo huo.
Shilingi milioni mia tatu siyo nyingi ukilinganisha na kiasi cha dhahabu ya
nusu kilo kinachopatikana kila siku kwani kiasi hicho kinaweza kuuzwa hadi
shilingi milioni 40 {nusu kilo ya dhahabu.
Wito
ni kwa watanzania wanaotaka kuwekeza wawasiliane na iMADS ili wapate taarifa
kamili na maandiko ya miradi ya jinsi ya kuwekeza katika madini aina ya dhahabu
kwani kitengo hiki cha chuo, kina taarifa zote muhimu za kibiashara za
uchumbaji wa dhahabu.
Pamoja
na maraha ya faida, hiyo huwa ni kwa wawekezaji, lakini kwa upande wa
wachimbaji wadogo wana machungu yao kama yalivyoshudiwa na mwandishi wa makala
hayo alipotembelea migodi na kujikuta analazimika kusaidia kusimamia shughuli
za maafa na majanga katika baadhi ya maeneo. Picha hapo chini zinaonesha
wachimbaji wadogo ambao wengi wao hawajajipanga, hawafuati taratibu za usalama
na kujiweka muda mwingi hatarini. Wachimbaji waliangukiwa na mgodi, walikaa
ndani ya shimo kwa siku tatu na siku ya nne tulifanikiwa kuwatoa wakiwa hoi,
bila chakula siku nne, bila maji na hewa kiduchu mno. Walikuwa hawana nguvu na
hawakuamini kuwa waliokolowa. Wachimbaji hao wadogo walidai kuwa kama
tusingelikuwepo sisi wageni, basi ingelikuwa mwisho wao kwani baadhi ya
wachimbai walikuwa na imani potofu kuwa, eti mgodi wenye maafa hutoa dhahabu
nyingi {hutapika dhahabu} kitu ambacho siyo cha kweli, kwani wachimbaji wengi
wanaofanikiwa ni wale wanaowatumia wataalam ao maafisa wa madini waliobobea
katika taaluma zao.
Kwa
taarifa zaidi na maelezo au kama una mchango wa mawezo wasiliana na
Dominickhaule@gmail.com Cell Phone:
0767 11 1173
MAJANGA YA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU TANZANIA
Wachimbaji wadogo wanye uwezo kiasi, wakiandaa mtambo tayari kwa kazi ya kutoa maji shimoni |
Ohooo! Asanteni Jamani. Sauti ya mchimbaji mdogo ilisikika kwa mbali |
Askari wa usalama akiwalinda majeruhi na kuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani na utulivy |
Majeruhi akipelekwa sehemu ya huduma ya kwanza |
Mchimbaji mdogo anaeshindwa kulia, akijaribu kushukuru kwa shida huku akipumua kwa tabu |
Majeruhi akitolewa shimoni alimokaa siku nne |
Mwandishi wa makala haya akisaidia kusimamia kikamilifu uokoaji |
Mmoja ya walionusurika kufa mgodini akiwahishwa kwa huduma ya kwanza |
KARAHA NA MARAHA YA WACHIMBAJI WADOGO
Wachimbaji
wadogo wa dhahabu wanapata dhahabu kwa namna mbili. Namna ya kwanza ni kama
vile wanaokota vipande vya dhahabu ambavyo kwa asilimia kubwa vinabeba dhahabu
na vinajulikana kwa jina la vikole {Alluvial Gold}, vipande hivi huweza kufikia
98% ya dhahabu na uchafu ukawa asilimia mbili tu. Asilimia hizo huwasilisha
kiwango au kiasi cha dhahabu kilichomo ndani kwa uwiano wa kipande kizima. Kitu
cha Ajabu kidogo katika uokotaji huu ni matokeo ya nyakati tofauti yanayofanya
aneo Fulani lifurike ghafla dhahabu nyingi za vipande au vikole hasa katika
maeneo ya kingo za mito.
Ikitokea
sehemu imepata dhahabu ya aina hiyo ambayo mara nyingi ninakuwa ni kama vile
imeshushwa ghafla kutoka mbinguni, mtu wa kwanza kuiona na kuiokota kiasi
Fulani hata kama ni usiku, huwa haitaji kuwaarifu watu isipokuwa kwa namna ya
ajabu, ndani ya siku mbili unaweza kushangaa kuwa watu zaidi ya elfu 20
wanaweza kupatikana sehemu hiyo na isijulikane wamejuaje na wametoka wapi, ni
matokeo ya kama vile miujiza. Kitondo cha dhahabu kutokea ghafla huitwa rashi
{rush} inaelekea ni wachimbaji wadogo wanatumia neno hilo lenye asili ya
kiingereza linalomaanisha watu wengi kwa wakati mmoja kukimbilia sehemu
ilikoibuka dhahabu.
Tafiti
nyingi zinaonesha kuwa Tanzania ina madini mengi na dhahabu imeenea karibu
katika kila wilaya ikitofautiana kwa kiasi na kiwango tu. Wachimbaji wa dhahabu
hutumia vifaa duni ambavyo vinashangaza kwa jinsi vinavyoweza kuwafikisha chini
hadi kufikia urefu wa futi mia mbili {200} na wanaweza kwenda kulia na kushoto
hadi mita zaidi ya futi 200 tena. Wakati mwingine hukutana na wachimbaji
wengine ndani kwa ndani na wanaweza kuzua mapambano yenye kuhatarisha maisha.
Mashimo kwa juu kama picha zinavyoonesha huwa na size ndogo sana ya hadi mita
moja ya mraba.
Mashimo
hayo hufungwa mbao au miti {uharibufu wa mazingira} nyingi zinazojulikana kwa
jina la kichimbaji kama “Matimba”. Miti hii hufanya kazi ya kuzuia mashimo
yasibomoke kirahisi hasa wakati wachimbaji wakiwemo chini ya ardhi. Miongoni
mwa matatizo yanayoweza kutokea chini ya
ardhi ni pamoja na ukosefu wa hewa au kufika maeneo yanye hewa yanye sumu na
hapo wachimbaji hupoteza maisha. Mchimbaji anakuwa na tochi iliyofungwa
kichwani na mpira kwa lengo la kumsaidia mwanga ilia one vizuri. Huwa hawavai
vifaa vya usalama kama vile miwani maalum ya kulinda macho, kofia za plastic au
chuma na viatu maalum wa usalama ili kuliinda miguu isiumie. Unaweza kutizama
picha hapo juu.
Ujenzi
wa mashimo au migodi ya wachimbaji wadogo hujumuisha uchimbaji wa shimo lenyewe
ukubwa umeandikwa hapo juu, uwekeji wa miti, mbao au zege, uezekaji na matumizi
ya vifaa kama kamba na mipira ya kuingizia hewa na mipira ya kutolea maji.
Kwa
ushauri, au taarifa zaidi wasiliana kupitia dominickhaule@gmail.com
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)