Social Icons


Jumamosi, 28 Desemba 2013

Technolojia ya 'Green House'

Green House ikiwa na baadhi ya mazao yaliyolimwa nje yake.

Nyanya aina ya Anna F 1 Huwa inakuwa ndefu zaidi ya futi nane ili kubeba mavuno mengi
 
UJASIRIAMALI WA KILIMO CHA NYANYA AINA YA ANNA F 1
 
Nyanya aina ya Anna FI, imekuwa ni kivutio kikubwa kwa wakulima wa Tanzania. Baadhi ya sifa ya nyanya hizo zimeainishwa hapa chini: -

1. Nyanya za Anna F 1 zinastawi vizuri sana ndani ya Green House. Green House pamoja na mambo mengine, inazuia bacteria wasiofaa na wadudu wengine kuharibu nyanya, inazuia baadhi ya mionzi ya jua isiyofaa kuingia ndani na kuharibu nyanya. Green House ina sifa pia ya kuzifanya nyanya kukua kwa haraka na kutoa mazao bora. Ubara wa mazao ni changamoto kwa wakulima wengi wa tanzania.
 
2. Nyanya aina ya Anna F 1 ina sifa ya kutoharibika haraka. Ikiiva mchini ina uwezo wa kukaa hadi miezi mitatu bila kuharibika na ikivunwa ina weza kukaa hadi miezi mitatu bila kuoza. Mjasiriamali ana uwezo wa kuiuza pole pole.
 
3. Green House zina ukubwa wa aina tofauti, mfano kuna za ukubwa wa 8m x 15m, 8m x 30m, 16m x 30m na kuendelea. Inawezekana kuwa na ekari moja au zaidi ya green house.
 
4. Nyanya ya Anna F 1 ina sifa ya ubora wa kuuzika hata katika maeneo ya wawekazaji kama vile Geita Gold mine na Barrick.
 
5. Green House ina uwezo wa kuotesha miche kuanzia mia 600 hadi zaidi 1200 kulingana na ukubwa wa banda lenyewe.
 
6. Mche mmoja wa nyanya una uwezo wa kutoa kiasi cha kilo kumi cha nyanya hadi kilo 80. Kilo 80 ni aina nyingine ya nyanya siyo Anna F 1.
 
7. Green House inarudisha faida ndani ya msimu mmoja na msimu mmoja unavuna nyanya kwa muda wa miezi nane mfululizo.
 
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu: +255 767 11 1173.
 
Ujenzi wa Green Hous ya Mafunzo Tuangoma Temeke Dar es Salaam
 
Green House iliyojengwa na i'MADS Dar kwaajili ya Mafunzo


 

Maoni 2 :

  1. naomba kujua gharama za kutengeneza greenhouse

    JibuFuta
  2. Asante mkuu, je Ni gharama kiasi gani za kutengeneza green house Na durability kabla ya ukarabati wake. 0753064252

    JibuFuta

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates