Social Icons


Jumamosi, 17 Mei 2014

MACHIMBO YA CHUMA LIGANGA NA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA


FURSA ZINAZOKUJA NA UWEKEZAJI WA MRADI WA CHUMA NA MAKAA YA MAWE LUDEWA
Wajasiriamali wa Wilaya ya Ludewa na watanufaika na uwekezaji mkubwa wa mradi wa migodi ya chuma na makaa ya mawe unaotarajiwa kuanza mapema mwakani. Mradi huo mkubwa wa madini ya chuma uliopo katika kijiji cha Liganga wilayani Ludewa na Makaa ya Mawe yaliyopo katika kijiji cha Mchuchuma Nkomang’ombe wilayani humo ni miongoni mwa miradi mikubwa nchini itakayoleta maendeleo ya kasi katika Taifa hili linalosherehekea miaka takribani 50 ya uhuru wake.
Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka china katka Kampuni iiliyoingia Ubia na NDC zinasema kuwa aina hiyo ya uwekezaji utakaoanza kwa kuwa na wafanya kazi elfu tano {5000} katika machimbo ya chuma na elfu tano {5000} katika machimbo ya makaa ya mawe huwa na tabia ya kwavutia zaidi ya wakazi milioni moja {1,000,000} katika mazingira na maeneo ya mradi. Kwa maana hiyo basi, mradi huo ukikamilika utawavutia wakazi zaidi ya milioni moja katika maeneo yanayozunguka mradi huo.
Madhumuni ya makala haya ni kujarifu kuwaarifu na kuwahabarisha vijana na wajasiriamali wanaoishi katika wilaya ya Ludewa na mikoa ya jirani jinsi watakavyonufaika na uwekezaji huo mkubwa kwani imekuwa ni tabia sasa kwa baadhi ya watu kuwa walalamishi zaidi kuliko kufanya tathmini ya fursa zitakazokuja na uwekezaji huo mkubwa kuliko uwekezaji wowote nchini ukitoa uwekezaji katika mradi wa TAZARA ambao pia umejengwa na kudhaminiwa na nchi ya China.
Je? Ni namna gani fursa zinaweza kutazamwa katika uwekezaji huo mkubwa? Hapa chini ni mwanzo tu wa namna ya kuanza kuziangalia fursa zitakazokuja na uwekezaji wa mradi wa chuma na makaa ya mawe Nchini.
1.             Kutakuwa na wafanyakazi elfu kumi ambao wataajiriwa na kama kila familia itakuwa na watu watatu watatu tu nyumbani basi tunaongelea ujio wa watu wapatao elfu thelathini {30,000} watakaokuwa na mashikamano ya moja kwa moja na migodi na ajira. Hivyo sisi tuwatizame wafanyakazi hao elfu kumi tu na baadhi ya mahitaji yao ya moja kwa moja. Kama ifuatavyo:

-       Kila mfanyakazi atahitaji maziwa lita moja kila siku, mayai mawili, na nusu kuku kila siku. Bila kuangalia mahitaji mengine kwa jumla mahitaji yatakuwa kama ifuatavyo:
i.               Kutakuwa na mahitaji ya maziwa lita elfu kumi {10,000} kila siku
ii.              Kutahitajika mayai elfu ishirini {20,000} kila siku
iii.            Kutakuwa na mahitaji ya Nyama za kuku na kuku elfu tano {5,000} watakuwa wanahitajika kila siku.
Hiyo ni sehemu ndogo tu ya fursa za uwekezaji zitakazokuja una machimbo makubwa ya chuma na makaa yam awe. iMADS imefanya tathmini Ludewa na kugundua kuwa hakuna kuku wa kienyeji wala wa kisasa wa kutosha, na bei ya kuku mmoja inaanzia shilingi elfu 13 hadi elfu 20 kutegemea muuzaji na uzito wa kuku. Hakuna taxi hata moja, hakuna hotel za kisasa, hakuna nyumba za kupangisha wala maeneo ya starehe.
Hadi iMADS inaondoka wilayani Ludewa, kulikuwa na shamrashamra za kuweka sahihi mikataba baina ya wakandarasi na TANROADS ya kukarabati na kupanua barabara ili kutengeneza kiwango cha changarawe kwa dhumuni la kuwezesha vifaa vya wawekezaji vyenye uzito wa hadi tani 150 na urefu wa hadi mita 15 ambavyo vitahitaji barabara ya aina yake kuviwezesha vipite salama hadi migodini.
Makala hii itaendelea ili kuonesha fursa zaidi zitakazokuja na uwezi wa migodi ya chuma na makaa yam awe Ludewa.

Moja ya mitambo inayosubiri ukarabati wa barabara ya Itoni hadi manda na Mkiu hadi Liganga
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates