Social Icons


Ijumaa, 3 Januari 2014

KILIMO CHA ALIZETI TANZANIA


 
1. Alizeti inastawi maeneo mengi Tanzania hususani maeneo yote yanakostawi mahindi. Baadhi ya mikoa inakostawi sana alizeti ni pamoja na Singida, Sumbawanga, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Mtwara, Tanga na Dodoma.

2. Alizeti hupandwa mbegu punje moja moja

3. Mbegu ya alizeti hupandwa kwa kuzamishwa ichi moja chini ya ardhi

4. Umbali wa mbegu hadi mbegu ni futi moja au sentimeta 30,  kwa mbegu za kawaida na futi mbili mbegu hadi mbegu kwa mbegu zinazokuwa kubwa na kuzaa alizeti yenye mzingo mkubwa

5. Eka moja huweza kupandwa kiasi cha kilo mbili za alizeti.

6. Eka moja huweza kupandwa kati ya mbegu elfu kumi na tano (15,000) hadi mbegu elfu ishirini na tano (25,000) kutegemeana na aina ya alizeti iliyopandwa.

7. Shamba la alizeti huwa halifukuliwi chini sana kwani hulimwa hadi ichi 8 tu chini ya ardhi
8. Mbegu namba mbili (2) huwa ni kubwa zaidi na mbegu namba tano (5) huwa ni ndogo zaidi. Ukubwa wa namba huwakilisha udogo wa mbegu.
9.  Alizeti huweza kuchanganywa na mazao mengine kama vile soya, mahindi, kunde nk
10. Ardhi iliyo hadi ni Ph 5.5 inafaa kwa kilimo cha alizeti
11. Kuhusu mbolea wasiliana nasi lakini Nitrogen hufaa zaidi na potasium.
12. Kuhusu mavuno kwa eka, bei ya alizeti, kiasi cha mafuta kwa kila eka, kiasi cha mashudu kwa kila eka, kuhusu aina za mashine za kukamulia alizeti na bei zake pamoja na gharama zote za kulima hadi kuuza mafuta wasiliana nasi kupitia anuani ya hapo chini.
13. Tunaweza pia kuandika mchanganuo mzima wa Biashara ya kilimo cha alizeti au biashara ya kukamua na kuuza mafuta ya alizeti.
14.   Simu: +255 767 11 1173. Kwa Dominick Mkuu kitengo cha Ujasiriamali (i'MADS) – Iringa.

 

Maoni 4 :

  1. habari naomba uniandikie andiko mradi la zao la alizeti
    asante

    JibuFuta
  2. Habari, nahitaji msaada wa kuandikiwa andiko la mradi wa kilimo Cha zao la Alizeti!

    Contact (jumannebakari31@gmail.com)

    JibuFuta
  3. Naomba kuipata mchanganuo wa kilimo cha alizeti,pia bei ya machine ya kukamulia mafua ya alzet

    JibuFuta
  4. Samahani nilikuwa nimebanwa sana. Sasahivi tunaweza wasiliana + 255 767111173

    JibuFuta

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates