Social Icons


Jumatano, 21 Mei 2014

LUDEWA YAPATA BARABARA YA LAMI


Hatimae Ndondondo si chururu Ludewa.
Kwa kumbu kumbu zangu, Mheshimiwa Deo Filikunjombe Alikuja na vipau mbele viwili. Vipaumbele hivi vimemfanya mbunge huyu machachari kutamka bungeni maneno ambayo yamekuwa ni msingi wa mabadiliko wa mwenendo wa bunge letu na matokeo yake yatawafikiwa watanzania wengi ikiwa ni pamoja na wajasiriamali wa Ludewa ambao watashuhudia neema.
Neema hii itawapata wale tu ambao si walalamishi, wabishi na watu ambao hawaishi kuilaumi serikali kwa mambo mengi. Watakaofanya kazi watashuhudia mambo yafuatayo: -
1. Watapata fedha nyingi kutokana na kilimo, uvuvi na biashara kwani itakuwa ni gharama ndogo sana kusafirisha mzigo kutoka Mikoani hadi Ludewa na Ludewa hadi mikoani.
2.              Nauli za mabasi na gharama za kusafirisha mizigo zitashuka sana.
3.              Mzunguko wa fedha utaongezeka kwani Ludewa imekaa sehemu nyeti kuliko Songea na Mbinga, kwani umbali toka dar ni mdogo kulinganisha na maeneo hayo.
4.              Itakuwa ni rahisi sana kwa wadau waliooa Ludewa na Walioolewa Ludewa kurudi home kuwekeza pamoja na kwamba watarudi kuwekeza katika wakati mgumu kwani wajanja wanachukua maeneo kwa mamia ya maekari.
5.              Wafanya kazi elfu kumi wa migodi watafurahia usafiri mzuri wa lami kutoka manda hadi Ludewa.
6.              Aliyelala Usimwamshe kwani utalala wewe. Ludewa ni wilaya ndogo hivyo fursa hazitakuwa na muda mrefu zikiwa zimelala.
Habari katika picha zina maelezo ya kina.
Ki msingi wajasiriamali wa wilaya ya Ludewa na mikoa ya jirani, ni lazima tumshukuru Mungu na tujitahidi kutoziacha fursa ambazo zitakwisha baada ya muda mfupi kwani watu wenye upeo wameanza kuitazama na kuwekeza Ludewa kutoka pande zote Tanzania.
Imekuwa ni bahati kwani, hata katika Uchaguzi wa Nijeria, Wakati GoodLuck akiwa makamu wa Rais, baadhi ya wananchi walisema, pamoja na kuwa huyu ni mpole badi, tumpe tu urais kwani wakati mwingine nchi inaweza kuwa nzuri kwa kuongozwa na mtu mwenye jina zuri tu. Hata kwa Ludewa, Kwa mujibu wa maelezo ya Mhe. Kolimba Mwenyekiti wa CCM Wilaya aliweza sema kuwa, kila enzi ina wakati na mtu wake. Ki ukweli Mhe wa Mbunge wa Ludewa ana bahati.
Fikiria jinsi ukarabati wa barabara ulivyotakiwa uende haraka hadi km chini ya 250 kupewa wakandarasi wanne na wametakiwa kuimaliza ndani ya miezi miwili. Raha zaidi ilikuwa pale ambapo sherehe za kuweka sahihi mkataba wa kufanya matengenezo maalum kwa kiwango cha changarawe barabara ya kutoka Itoni Njombe kupitia Ludewa hadi Mchuchuma na Nyingine ya kuanzia Mkiu hadi Liganga zilikuwa zimeanza kazi. Ni jambo la kufurahisa kuona mkandarasi makini Boimanda aliweka seti nne za vifaa maeneo tafauti tofauti kati ya Itoni na Mkiu {seti moja ni Grader, Excavator, na Roller Compactor} na vilianza kazi kabla ya kuweka sahihi mkataba.
Maelezo ya picha pamoja na mambo mengine yanaonesha ushuhuda wa watu mbali mbali wakati wa kuweka sahihi mkataba huo.
Habari ya furaha kwa wajasiriamali wa Ludewa inaongezeka ndani ya wiki mbili baada ya kushuhudia upanuzi wa barabara kiwango cha lami, sasa wanapewa km 50 kwa kiwango cha lami. Ikumbukwe, Tayari Ludewa mjini kuna ujenzi unaendelea wa Km 10 za barabara ya Lami Kuzunguka takribani mitaa yote ya Ludewa. Wajasiriamali wa Ludewa Mungu awape nini. ANGALIA PICHA HAPO CHINI. Habari na Picha na {I’MADS}

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates