Moja
ya maeneo yenye fursa nzuri za ujasiriamali ni eneo la uchimbaji mdogo wa
dhahabu. Uchimbaji wa dhahabu wa asili, unafanywa na wachimbaji wadogo ambao
wengi wao hawajui wala hawataki kizifahamu sheria za madini nchini. iMADS
imepata fursa ya kufahamu mambo muhimu ya ki-uwekezaji katika eneo hili ambalo
lina chungu zenye tamu.
Imeonekana
ni vema kuandika mfululizo wa baadhi ya taarifa za msingi zinazoweza kuwasaidia
wachimbaji wadogo, wadau, maafisa wa serikali na wawekezaji wengine watarajiwa
wanaopenda kuwekeza katika eneo hili. Baadhi ya taarifa zenye raha zitahuzu
namna ya Wachimbaji wenyewe, maeneo ya uchimbaji wa dhahabu, changamoto tatu za
uchimbaji, aina za vifaa vya ki-asili na vya kisasa vya uchimaji, kiasi cha
dhahabu inayoweza kupatikana kwa siku kwa mchimbaji, jinsi maisha ya uchimbaji
yalivyo na hatari zake pamoja na masoko na namna uchimbaji wa dhahabu
unavyofanyika na jinsi dhahabu nyingi ilivyokuwa ikiuzwa nje ya nchi bila ya
Taifa kupata baadhi ya mapato. Mwisho makala itazungumzia madhara na athari za
uuzaji wa dhahabu nje ya nchi bila ya kuihusisha serikali. Kwani mwisho wa
siku, kila upande unapoteza faida za mapato ya rasilimali hii. Nchi kama Afrika
ya Kusini, Dhahabu ni nyara na mali ya serikali na serikali pamoja na wananchi
wanapata manufaa makubwa ya dhahabu kwa kushirikishana.
Makala
itaandika pia kuhusu maisha ya ujumla ya wachimbaji wadogo na jinsi walivyo na
matumizi mabaya licha ya kufanya kazi inayogharimu maisha yao, katu wengi wao
hawajapiga hatua za ki-maendeleo ya ki-uchumi. Fuatilia habari hizi na picha
kila siku. Picha ya kwanza hapo chini inamuonesha mchimbaji aliyena furaha
akitokea ndani ya shimo ambalo huweza kuishi humo kwa zaidi ya siku saba bila
kutoka nje.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni