Wachimbaji
wadogo wa dhahabu wanapata dhahabu kwa namna mbili. Namna ya kwanza ni kama
vile wanaokota vipande vya dhahabu ambavyo kwa asilimia kubwa vinabeba dhahabu
na vinajulikana kwa jina la vikole {Alluvial Gold}, vipande hivi huweza kufikia
98% ya dhahabu na uchafu ukawa asilimia mbili tu. Asilimia hizo huwasilisha
kiwango au kiasi cha dhahabu kilichomo ndani kwa uwiano wa kipande kizima. Kitu
cha Ajabu kidogo katika uokotaji huu ni matokeo ya nyakati tofauti yanayofanya
aneo Fulani lifurike ghafla dhahabu nyingi za vipande au vikole hasa katika
maeneo ya kingo za mito.
Ikitokea
sehemu imepata dhahabu ya aina hiyo ambayo mara nyingi ninakuwa ni kama vile
imeshushwa ghafla kutoka mbinguni, mtu wa kwanza kuiona na kuiokota kiasi
Fulani hata kama ni usiku, huwa haitaji kuwaarifu watu isipokuwa kwa namna ya
ajabu, ndani ya siku mbili unaweza kushangaa kuwa watu zaidi ya elfu 20
wanaweza kupatikana sehemu hiyo na isijulikane wamejuaje na wametoka wapi, ni
matokeo ya kama vile miujiza. Kitondo cha dhahabu kutokea ghafla huitwa rashi
{rush} inaelekea ni wachimbaji wadogo wanatumia neno hilo lenye asili ya
kiingereza linalomaanisha watu wengi kwa wakati mmoja kukimbilia sehemu
ilikoibuka dhahabu.
Tafiti
nyingi zinaonesha kuwa Tanzania ina madini mengi na dhahabu imeenea karibu
katika kila wilaya ikitofautiana kwa kiasi na kiwango tu. Wachimbaji wa dhahabu
hutumia vifaa duni ambavyo vinashangaza kwa jinsi vinavyoweza kuwafikisha chini
hadi kufikia urefu wa futi mia mbili {200} na wanaweza kwenda kulia na kushoto
hadi mita zaidi ya futi 200 tena. Wakati mwingine hukutana na wachimbaji
wengine ndani kwa ndani na wanaweza kuzua mapambano yenye kuhatarisha maisha.
Mashimo kwa juu kama picha zinavyoonesha huwa na size ndogo sana ya hadi mita
moja ya mraba.
Mashimo
hayo hufungwa mbao au miti {uharibufu wa mazingira} nyingi zinazojulikana kwa
jina la kichimbaji kama “Matimba”. Miti hii hufanya kazi ya kuzuia mashimo
yasibomoke kirahisi hasa wakati wachimbaji wakiwemo chini ya ardhi. Miongoni
mwa matatizo yanayoweza kutokea chini ya
ardhi ni pamoja na ukosefu wa hewa au kufika maeneo yanye hewa yanye sumu na
hapo wachimbaji hupoteza maisha. Mchimbaji anakuwa na tochi iliyofungwa
kichwani na mpira kwa lengo la kumsaidia mwanga ilia one vizuri. Huwa hawavai
vifaa vya usalama kama vile miwani maalum ya kulinda macho, kofia za plastic au
chuma na viatu maalum wa usalama ili kuliinda miguu isiumie. Unaweza kutizama
picha hapo juu.
Ujenzi
wa mashimo au migodi ya wachimbaji wadogo hujumuisha uchimbaji wa shimo lenyewe
ukubwa umeandikwa hapo juu, uwekeji wa miti, mbao au zege, uezekaji na matumizi
ya vifaa kama kamba na mipira ya kuingizia hewa na mipira ya kutolea maji.
Kwa
ushauri, au taarifa zaidi wasiliana kupitia dominickhaule@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni