Social Icons


Ijumaa, 20 Juni 2014

MAJANGA NA MARAHA YA WACHIMBAJI WADOGO TANZANIA


Mwandishi wa makala haya amebahatika kupata baadhi ya taarifa nyingi za uchimbaji na wachimbaji wadogo ambao baadhi yao huamini kuwa kuna sehemu ya ushirikina inatumika jambo ambalo wataalam wanalipinga vikali. Wachimbaji wadogo wa dhahabu ambao nchini idadi yao inakaribia milioni tatu 3,000,000 wamekuwa na changamoto kubwa tatu: -
i.                Tatizo la Kujaa maji migodi yao (mashapo au shafts}
ii.              Tatizo la Mwamba mgumu wanaoukabili ndani ya mgodi na jinsi ya kuutoa baada ya kuuvuja
iii.             Tatizo la mtaji
Wakati utatuzi wa tatizo au changamoto ya kwanza ni kuitatua kwa kupata pampu za maji zenye uwezo wa kutoa maji haraka wakati uchimbaji unaendelea, tatizo la pili la mwamba linatatuliwa na mashine za kisasa za kupasulia miamba {jack hammers na compressors} ambavyo vyote vinahitaji uwekezaji mkubwa kuzidi uwezo wao. Tatizo la kutoa mwamba au vipande vya mawe na udongo wenye dhahabu linatatuliwa kwa kupata mshine ya kunyanyulia mizigo aina ya {crane} zinye uwezo wa tani moja na kuendelea kwani kwa kutumia ndoo, inawachukua matumizi ya nguvu nyingi na muda mrefu sana. Mashine zingeliwawezesha kutoa kiasi kikubwa cha udongo na mawe kwa muda mfupi na kufanya kazi ya kusaga kwa muda mrafu wakiwa namali ghafi nyingi katika stoo zao.
Kuna faida kubwa pia katika uchimbaji mdogo licha ya kuwa na changamoto mbali mbali kwani kwa mchimbaji aliyejipanga anakuwa na uwezo wa kuzalisha hadi kilo moja kila siku. Mwandishi wa makala haya alitembelea mgodi mmoja wa mchimbaji mdogo ambaye uwezo wake ulikuwani nusu kilo ya dhababu kwa siku. Uwekezaji unaweza kutumia kiasi cha shilingi milioni mia tatu 300,000,000/= kwa wachimbaji wadogo wenye uwezo na wanaofuata utaalamu kwani maafisa madini wana taaluma nzuri ya kushauri masuala ya uchimbaji na kumuwezesha mchimbaji mdogo kufikia uwezo huo. Shilingi milioni mia tatu siyo nyingi ukilinganisha na kiasi cha dhahabu ya nusu kilo kinachopatikana kila siku kwani kiasi hicho kinaweza kuuzwa hadi shilingi milioni 40 {nusu kilo ya dhahabu.
Wito ni kwa watanzania wanaotaka kuwekeza wawasiliane na iMADS ili wapate taarifa kamili na maandiko ya miradi ya jinsi ya kuwekeza katika madini aina ya dhahabu kwani kitengo hiki cha chuo, kina taarifa zote muhimu za kibiashara za uchumbaji wa dhahabu.
Pamoja na maraha ya faida, hiyo huwa ni kwa wawekezaji, lakini kwa upande wa wachimbaji wadogo wana machungu yao kama yalivyoshudiwa na mwandishi wa makala hayo alipotembelea migodi na kujikuta analazimika kusaidia kusimamia shughuli za maafa na majanga katika baadhi ya maeneo. Picha hapo chini zinaonesha wachimbaji wadogo ambao wengi wao hawajajipanga, hawafuati taratibu za usalama na kujiweka muda mwingi hatarini. Wachimbaji waliangukiwa na mgodi, walikaa ndani ya shimo kwa siku tatu na siku ya nne tulifanikiwa kuwatoa wakiwa hoi, bila chakula siku nne, bila maji na hewa kiduchu mno. Walikuwa hawana nguvu na hawakuamini kuwa waliokolowa. Wachimbaji hao wadogo walidai kuwa kama tusingelikuwepo sisi wageni, basi ingelikuwa mwisho wao kwani baadhi ya wachimbai walikuwa na imani potofu kuwa, eti mgodi wenye maafa hutoa dhahabu nyingi {hutapika dhahabu} kitu ambacho siyo cha kweli, kwani wachimbaji wengi wanaofanikiwa ni wale wanaowatumia wataalam ao maafisa wa madini waliobobea katika taaluma zao.
Kwa taarifa zaidi na maelezo au kama una mchango wa mawezo wasiliana na
Dominickhaule@gmail.com Cell Phone: 0767 11 1173

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates