Tanzania ni nchi ya pili kuuza Asali kwa wingi nchi za nje baada ya Ethiopia. Ethiopia inaongoza katika Afrika kwa uuzaji wa asali nchi za nje lakini ni kama vile imekwishayamaliza maeneo yote yanayofaa kufuga nyuki. Wakati Tanzania imetumia chini ya asilimia 10 ya maeneo yote yanayofaa kufuga nyuki.
Dunia sasahivi imekuwa na matumizi makubwa ya mazao ya nyuki na maeneo mengi yanatumia mazao ya nyuki katika shughuli mbali mbali. Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na matumizi ya kutengenezea madawa, matumizi katika kuoka mikate, kwenye vyakula na matumizi ya kutengeneza bidhaa kama vile mishumaa.
Taasisi ya Decision Foundation inajenga uwezo kupitia makongamano mbali mbali na semina hususani katika kuyatambua mazao ya nyuki kama vile Sumu ya Nyuki, Maziwa ya Nyuki, Nta, Polen na Asali yenyewe.
Tunawaunganisha pia watu wenye nia, dhamira, hitaji na mitaji ili wafanye ufugaji katika eneo moja. Kupitia utaratibu maalumu, Decision Foundation ambayo ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa kwaajili ya kuwajengea uwezo wasichana, wanawake, vijana na wajasiriamali ina uwezo wa kupata maeneo, vifaa, soko na pia huwaunganisha wajasiriamali ili wafanye miradi ya pamoja. Kufanya miradi kwa pamoja kunasaidia kupunguza gharama za uendeshaji.
Kwa maelezo zaidi piga simu +255 767 11 1173