Social Icons


Ijumaa, 20 Juni 2014

KARAHA NA MARAHA YA WACHIMBAJI WADOGO


Wachimbaji wadogo wa dhahabu wanapata dhahabu kwa namna mbili. Namna ya kwanza ni kama vile wanaokota vipande vya dhahabu ambavyo kwa asilimia kubwa vinabeba dhahabu na vinajulikana kwa jina la vikole {Alluvial Gold}, vipande hivi huweza kufikia 98% ya dhahabu na uchafu ukawa asilimia mbili tu. Asilimia hizo huwasilisha kiwango au kiasi cha dhahabu kilichomo ndani kwa uwiano wa kipande kizima. Kitu cha Ajabu kidogo katika uokotaji huu ni matokeo ya nyakati tofauti yanayofanya aneo Fulani lifurike ghafla dhahabu nyingi za vipande au vikole hasa katika maeneo ya kingo za mito.
Ikitokea sehemu imepata dhahabu ya aina hiyo ambayo mara nyingi ninakuwa ni kama vile imeshushwa ghafla kutoka mbinguni, mtu wa kwanza kuiona na kuiokota kiasi Fulani hata kama ni usiku, huwa haitaji kuwaarifu watu isipokuwa kwa namna ya ajabu, ndani ya siku mbili unaweza kushangaa kuwa watu zaidi ya elfu 20 wanaweza kupatikana sehemu hiyo na isijulikane wamejuaje na wametoka wapi, ni matokeo ya kama vile miujiza. Kitondo cha dhahabu kutokea ghafla huitwa rashi {rush} inaelekea ni wachimbaji wadogo wanatumia neno hilo lenye asili ya kiingereza linalomaanisha watu wengi kwa wakati mmoja kukimbilia sehemu ilikoibuka dhahabu.
Tafiti nyingi zinaonesha kuwa Tanzania ina madini mengi na dhahabu imeenea karibu katika kila wilaya ikitofautiana kwa kiasi na kiwango tu. Wachimbaji wa dhahabu hutumia vifaa duni ambavyo vinashangaza kwa jinsi vinavyoweza kuwafikisha chini hadi kufikia urefu wa futi mia mbili {200} na wanaweza kwenda kulia na kushoto hadi mita zaidi ya futi 200 tena. Wakati mwingine hukutana na wachimbaji wengine ndani kwa ndani na wanaweza kuzua mapambano yenye kuhatarisha maisha. Mashimo kwa juu kama picha zinavyoonesha huwa na size ndogo sana ya hadi mita moja ya mraba.
Mashimo hayo hufungwa mbao au miti {uharibufu wa mazingira} nyingi zinazojulikana kwa jina la kichimbaji kama “Matimba”. Miti hii hufanya kazi ya kuzuia mashimo yasibomoke kirahisi hasa wakati wachimbaji wakiwemo chini ya ardhi. Miongoni mwa  matatizo yanayoweza kutokea chini ya ardhi ni pamoja na ukosefu wa hewa au kufika maeneo yanye hewa yanye sumu na hapo wachimbaji hupoteza maisha. Mchimbaji anakuwa na tochi iliyofungwa kichwani na mpira kwa lengo la kumsaidia mwanga ilia one vizuri. Huwa hawavai vifaa vya usalama kama vile miwani maalum ya kulinda macho, kofia za plastic au chuma na viatu maalum wa usalama ili kuliinda miguu isiumie. Unaweza kutizama picha hapo juu.
Ujenzi wa mashimo au migodi ya wachimbaji wadogo hujumuisha uchimbaji wa shimo lenyewe ukubwa umeandikwa hapo juu, uwekeji wa miti, mbao au zege, uezekaji na matumizi ya vifaa kama kamba na mipira ya kuingizia hewa na mipira ya kutolea maji.
Kwa ushauri, au taarifa zaidi wasiliana kupitia dominickhaule@gmail.com

KARAHA NA MARAHA YA UCHIMBAJI MDOGO

Shimo lililofunikwa likionekana pamoja na eneo la uchimbaji lenye leseni PML

Shimo au shap lililofunikwa na nailoni kuzuia mvua na maji yasiingie shimoni kwa usalama
Shaft au Shapo la miti lenye kamba za kutolea Udongo kwa ndoo

Shaft au Shapo la Mbao lenye mabomba ya kutolea maji nje ya shimo

KARAHA NA MARAHA YA UCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU


Moja ya maeneo yenye fursa nzuri za ujasiriamali ni eneo la uchimbaji mdogo wa dhahabu. Uchimbaji wa dhahabu wa asili, unafanywa na wachimbaji wadogo ambao wengi wao hawajui wala hawataki kizifahamu sheria za madini nchini. iMADS imepata fursa ya kufahamu mambo muhimu ya ki-uwekezaji katika eneo hili ambalo lina chungu zenye tamu.
Imeonekana ni vema kuandika mfululizo wa baadhi ya taarifa za msingi zinazoweza kuwasaidia wachimbaji wadogo, wadau, maafisa wa serikali na wawekezaji wengine watarajiwa wanaopenda kuwekeza katika eneo hili. Baadhi ya taarifa zenye raha zitahuzu namna ya Wachimbaji wenyewe, maeneo ya uchimbaji wa dhahabu, changamoto tatu za uchimbaji, aina za vifaa vya ki-asili na vya kisasa vya uchimaji, kiasi cha dhahabu inayoweza kupatikana kwa siku kwa mchimbaji, jinsi maisha ya uchimbaji yalivyo na hatari zake pamoja na masoko na namna uchimbaji wa dhahabu unavyofanyika na jinsi dhahabu nyingi ilivyokuwa ikiuzwa nje ya nchi bila ya Taifa kupata baadhi ya mapato. Mwisho makala itazungumzia madhara na athari za uuzaji wa dhahabu nje ya nchi bila ya kuihusisha serikali. Kwani mwisho wa siku, kila upande unapoteza faida za mapato ya rasilimali hii. Nchi kama Afrika ya Kusini, Dhahabu ni nyara na mali ya serikali na serikali pamoja na wananchi wanapata manufaa makubwa ya dhahabu kwa kushirikishana.
Makala itaandika pia kuhusu maisha ya ujumla ya wachimbaji wadogo na jinsi walivyo na matumizi mabaya licha ya kufanya kazi inayogharimu maisha yao, katu wengi wao hawajapiga hatua za ki-maendeleo ya ki-uchumi. Fuatilia habari hizi na picha kila siku. Picha ya kwanza hapo chini inamuonesha mchimbaji aliyena furaha akitokea ndani ya shimo ambalo huweza kuishi humo kwa zaidi ya siku saba bila kutoka nje.

KARAHA NA MARAHA YA UCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU

Mchimbaji Mdogo akitoka nje ya shimo lake. {shaft au shapo}

Jumanne, 10 Juni 2014

DECISION FOUNDATION YATOA MAFUNZO YA UJASIRIMALI KIBAHA

Mkufunzi akitoa maelezo ya jinsi ya kuanzisha Biashara kwa wafanya kazi wa Kibaha

Mkufunzi Dominick Haule Akijibu Maswali ya Wafanyakazi wa Shirika la Elimu Kibaha wakati wa Mafunzo ya Ujasiriamali

Mama Gowele anayefanya kazi Hospitali ya Tumbi Kibaha akiwaonesha matunda wakufunzi. Yalitoka shambani kwake

Walimu wa Kibaha wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali yaliyokuwa yakitolewa na Decision Foundation

Walimu wa Kibaha wakifuatilia Mafunzo ya Ujasiriamali

Alhamisi, 5 Juni 2014

MAFUTA YA UFUTA NI MAZURI KWA AFYA

Mafuta ya Ufuta yaliyochujwa vizuri

Chupa ya Mafuta ya Ufuta
 

FAIDA YA MAFUTA YA UFUTA

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana matatizo ya kiafya yanayowakabili wajasiriamali na watu wengi kwa ujumla. Katika kusoma soma vitabu na taarifa nyingi katika mtandao nimepata taarifa nzuri ambazo zitawasaidia vijana na wajasiriamali watakaoamua kuwekeza katika kilimo na uzalishaji wa mafuta ya ufuta ambayo yanaheshimika duniani kote. Makala hii imeandikwa kwa kuperuzi vitabu na mitandao na inaweza kuwa nzuri zaidi kama itatumiwa kwa kushirikisha madaktari na wataalam mbali mbali. Ifuatayo ni taarifa niliyoipata katika mitandao na chanzo cha taarifa hii imo kimewekwa hapo chini, 

Sesame Oil Benefits/FAIDA ZA MAFUTA YA UFUTA

The health benefits of sesame are amazing. In fact, this nutrient dense food is been used for over 5000 years. Many consider sesame oil a medicinal food and its use has grown in popularity. As a matter of fact, sesame oil can provide benefits for your skin, teeth and bones as well as other health benefits.
Maajabu ya kiafya ya mafuta ya Ufuta yanashangaza. Mafuta ya ufuta yenye virutubisho muhimu yamekuwa yakitumika tangu miaka 5000 iliyopita. Matumizi ya mafuta ya ufuta yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na umaarufu wake kuongezeka kwa kuwa wengi wanaamini kuwa ni dawa kutokana na unafuu utokanao na maradhi mbali mbali. Kuna ukweli uliothibitika kuwa, mafuta ya ufuta yanasaidia sana matatizo ya ngozi, meno, na mifupa pamoja na kuwa na manufaa mengine mengi.
Nutritional Facts of Sesame Oil/Virutubisho vilivyomo katika mafuta ya ufuta
Nutrients
Amount Per Ounce (28g)
Manganese
0.7 mg, 35% RDA
Copper
0.7 mg, 35% RDA
Calcium
277 mg, 28% RDA
Iron
4.1 mg, 23% RDA
Magnesium
99.7 mg, 25% RDA
Zinc
2 mg, 13% RDA
Fiber
3.9 g, 16% RDA
Thiamine
0.2 mg, 15% RDA
Vitamin B6
0.2 mg, 11% RDA
Phosphorus
179 mg, 18% RDA
Magnesium
4.1 mg, 20% RDA
Zinc
99.7 mg, 25% RDA
Tryptophan
2 mg, 13% RDA
Fiber
93 mg, amino acid
Protein
4.7g
Benefits of Sesame Oil
1. Beautiful and Healthy Skin
Collagen is the structural backbone of healthy skin. The zinc in sesame seeds can boost collagen production, resulting in more elastic and smooth appearing skin. Research also shows that zinc is beneficial in the body’s repair processes and can soothe burns as well as other skin conditions.
Mafuta ya ufuta ni muhimu kwa afya ya ngozi. Mafuta ya ufuta yanasaidia pia kupunguza ngozi isiunguzwe na jua.

2. Oral Health
Sesame oil has been shown to reduce plaque and whiten teeth. The technique of swishing sesame oil in the mouth, oil pulling, boosts oral health by decreasing the harmful bacteria (Streptococcus mutants).
Mafuta ya ufuta yanatakatisha meno na kuua bacteria mdomoni
3. Diabetes Prevention
Sesame oil has been shown to decrease both blood pressure and glucose in patients with both diabetes and high blood pressure. The magnesium and other nutrients in sesame seeds were shown by the American Journal of Clinical Nutrition to improve the effectiveness of the oral diabetic treating drug glibenclamide in type 2 diabetic patients.
Mafuta ya ufuta yanapunguza shinikizo la damu na kuwasaidia wagonjwa wa kisukari
4. Reducing Blood Pressure
The rich magnesium content of sesame seeds have been shown to lower blood pressure in hypertensive diabetics.
Mafuta ya ufuta yanasaidia kupunguza shinikizo la damu kwa wagonjwa wa kisukari.
5. Heart Health
Heart disease is partially caused by free radicals and oxidative stress. Sesame seeds contain sesamol, a potent antioxidant and anti-inflammatory compound, known to be beneficial in battling heart disease and atherosclerosis. Research has revealed that sesamol contains of two dozen helpful pharmacologic properties.
Mafuta ya ufuta yanawasaidia pia wagonjwa wa moyo
6. Protection Against Radiation
We are all exposed to radiation whether we realize it or not. UV rays hit us whenever we go outside and there exists a constant level of background radiation wherever you live. Sesame seeds help our bodies protect themselves from DNA damage due to radiation. Several studies on mice exposed to radiation showed that those ingesting sesame seeds (sesamol) had longer lives that those mice that didn’t consume sesamol.
Mafuta ya ufuta yanapunguza madhara ya mionzi mibaya kutoka juani na yanasaidia kwa kulinda vinasaba {DNA} mwilini visiharibike kirahisi
7. Cancer Prevention
Sesame seeds are believed to possess anti-cancer properties. Research from the American Journal of Clinical Nutrition reported that magnesium intake decreased the risk of colorectal cancer. Their data noted that for every 100 mg intake of magnesium, the risk of colorectal cancer decreased by approximately 12%.
Mafuta ya ufuta yanasaidia kama kinga kwa kiasi Fulani kwa ugonjwa wa kansa
8. Bone Health
The high content of both zinc and calcium in sesame seeds is a powerful tool to help combat osteoporosis. Deficiency of either of this can increase the risk of hip and spine fractures. Fortunately, taking sesame seeds can boost bone mineral density.
Mafuta ya ufuta yanasaidia kuongeza uimara wa mifupa mwilini
9. Digestive Health
Fiber is a key dietary ingredient for proper digestive health. Sesame seeds are loaded with fiber and vital for improving and maintaining colon health.
Mafuta ya ufuta yanasaidia uyeyushaji wa chakula kwa kiasi Fulani pamoja na kusaidia kulinda utumbo usipate maradhi kirahisi
10. Rheumatoid Arthritis Relief
The copper found in sesame seeds is important for strengthening tissues such as blood vessels and joints. Those suffering from rheumatoid arthritis can experience a decrease in pain and joint swelling due to the anti-inflammatory effects of the copper contained in sesame seeds.
Mafuta ya ufuta yanaimarisha mishipa na misuli mwilini. Hupunguza pia maumivu ya viongo vya mwili
11. Respiratory Health and Asthma Prevention
Magnesium is used to decrease the severe spasm in bronchiole tubes by physicians worldwide. The rich magnesium content of sesame seeds can be helpful for those suffering respiratory problems.
Mafuta ya ufuta yanawasaidia pia wenye matatizo ya kupumua
12. Antiviral and Antibacterial
The power of sesame seed oil has the document for centuries. In Ayurvedic medicine it has much significance and practitioners believe that sesame seed oil has antibacterial and antifungal properties. Holistic medicine practitioners use sesame seed oil to treat strep throat, staphylococcus bacteria and also athlete’s foot. It’s important to note that the FDA does not recommend sesame seed oil for medicinal purposes and that clinical studies, at this point, are lacking. 
13. Other Benefits
Ancient Chinese and Ayurvedic practitioners utilized sesame oil to combat a variety of inflammatory, infectious and cancer causing processes. Sesame oil is believed to relieve pain syndromes such as tendonitis, bursitis, arthritis, colitis, irritable bowel syndrome and GERD. It can also reduce stress, lower cholesterol and detoxify the body.
Tangu enzi za mababu wachina wamekuwa wakitumia mafuta ya ufuta kama kinga kwa maradhi mbali mbali.
Ni vizuri kuwasiliana na madactari kuhusiana na makala hiyo hapo juu. Kwa ushauri tu, mwandishi wa makala haya nimekuwa nikitumia mafuta ya ufuta kwa mwaka sasa. Yamenisaidia sana kupunguza maumivu ya misuli kabla na baada ya mazoezi. Maumivu ya misuli yanapungua nikitumia mafuta ya ufuta kwa kupaka vizuri kiasi cha kutosha.
UKIHITAJI MAFUTA YA UFUTA, Wasiliana na:
Mobile: 255 767 11 1173.
Email:dominickhaule@gmail.com




 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates