Social Icons


Jumatano, 1 Januari 2014

KILIMO CHA MAHINDI TANZANIA

Mahindi yaliyopandwa kitaalam ni chanzo cha Faida kubwa


Ni muhimu kupanda mahindi kwa vipimo mbegu hadi mbegu na mstari hadi mstari

Katika ujasiriamali, ni wale tu watakaofanya kazi kwa bidii na kutumia utaalam watafanikiwa. Kilimo cha mahidi kinahitaji kufanyiwa maandalizi mazuri ikiwa ni pamoja na mambo yafuatayo: -
 
1. Ni vizuri kupima udongo shambani kabla ya kuanza kilimo. Utambuzi wa hali ya hewa ni muhimu pia kwani kwa wanaotegemea mvua ni vizuri kulima mahindi maeneo ambayo mvua hunyesha kwa uhakika. Namna ya kupima udogo na mahali pa kupima udongo i'MADS itashauri.
 
2. Shamba la mahindi hupandwa mbegu umbali wa sentimita 30 kutoka mbegu hadi mbegu.
 
3. Umbali wa mstari hadi mstari katika shamba la mahindi huwa ni kati ya sentimeta sitini na 95 kutegemea aina ya mbegu.
 
4. Eka moja ya shamba la Mahindi lenye urefu na mapana ya mita 70 kwa 70 linategemewa kutoa au kuoteshwa miche kati ya 54.424 na miche 55,000 kutegemea aina ya mbegu iliyopandwa.
 
6. Kwa wale wasio na mashamba makubwa, wana weza kupata kati ya shilingi za kitanzania milioni  tano hadi milioni 10 kwa eka moja kutegemea aina ya mbegu, idadi ya mahindi katika kila mche na kama watakuwa wameuza mahindi yakiwa mabichi kwa kati ya shilingi mia moja kwa mhindi mmoja hadi shilingi mia tano kwa mhindi mmoja mbichi.
 
7. Mahindi makavu kwa shamba lolote lililolimwa kitaalam linategemewa kutoa mavuno ya magunia ya kiasi cha kilo mia yasiyopungua arubaini.
 
8. Ujasiriamali mzuri wowote huanza na maandishi katika karatasi. Ni muhimu kabla ya kulima mahindi mjasiriamali aainishe katika karatasi mambo yafuatayo ili ajue faida au hasara ya kiasi gani ataitarajia; Gharama za kununua au kukodi shamba, gharama za kulima, mbegu, palizi, mbolea, madawa ya wadudu, kuvuna, kuweka katika vifungashio au magunia, usafirishaji, madawa ya kuhifadhia mahindi, gharama za kuhifadhi na gharama za kufikisha sokoni. Hayo yanatakiwa yazingatiwe kabla hata ya kununua au kukodi shamba ili kuwa na uhakika.
 
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu +255 767 11 1173.

Maoni 4 :

  1. nimelipenda sana chapisho hili najua nimejifunza mengi kwa maandishi machache yaliyoandikwa natarajia kufanya kazi hii kuanzia mwaka huu. nashukuru kwa muongozo

    JibuFuta
  2. Nimefuatilia sana kipindi chako kupitia Knowledgetv(ESRF) na nimeelimika kwa kiasi fulani. mimi ninaishi dar es salaam, je nawezaje kupata mafunzo au kujiunga na mafunzo ya ujasialiamali nikiwa huku? au mnatoa huduma zenu dar es salaam?

    JibuFuta
  3. Safi Tunamshukuru maana hata hivi inatakiwa tukulipe. Endelea kunisaidia

    JibuFuta
  4. Nimependa kumbe ukilima vizuri unaweza kupata kati ya gunia arobaini kwa ekari moja.

    JibuFuta

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates