FURSA ZINAZOKUJA NA UWEKEZAJI WA MRADI WA CHUMA NA MAKAA YA MAWE LUDEWA
Wajasiriamali wa Wilaya ya Ludewa na watanufaika
na uwekezaji mkubwa wa mradi wa migodi ya chuma na makaa ya mawe unaotarajiwa
kuanza mapema mwakani. Mradi huo mkubwa wa madini ya chuma uliopo katika kijiji
cha Liganga wilayani Ludewa na Makaa ya Mawe yaliyopo katika kijiji cha
Mchuchuma Nkomang’ombe wilayani humo ni miongoni mwa miradi mikubwa nchini
itakayoleta maendeleo ya kasi katika Taifa hili linalosherehekea miaka
takribani 50 ya uhuru wake.
Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka china katka
Kampuni iiliyoingia Ubia na NDC zinasema kuwa aina hiyo ya uwekezaji utakaoanza
kwa kuwa na wafanya kazi elfu tano {5000} katika machimbo ya chuma na elfu tano
{5000} katika machimbo ya makaa ya mawe huwa na tabia ya kwavutia zaidi ya
wakazi milioni moja {1,000,000} katika mazingira na maeneo ya mradi. Kwa maana
hiyo basi, mradi huo ukikamilika utawavutia wakazi zaidi ya milioni moja katika
maeneo yanayozunguka mradi huo.
Madhumuni ya makala haya ni kujarifu
kuwaarifu na kuwahabarisha vijana na wajasiriamali wanaoishi katika wilaya ya
Ludewa na mikoa ya jirani jinsi watakavyonufaika na uwekezaji huo mkubwa kwani
imekuwa ni tabia sasa kwa baadhi ya watu kuwa walalamishi zaidi kuliko kufanya
tathmini ya fursa zitakazokuja na uwekezaji huo mkubwa kuliko uwekezaji wowote
nchini ukitoa uwekezaji katika mradi wa TAZARA ambao pia umejengwa na
kudhaminiwa na nchi ya China.
Je? Ni namna gani fursa zinaweza
kutazamwa katika uwekezaji huo mkubwa? Hapa chini ni mwanzo tu wa namna ya
kuanza kuziangalia fursa zitakazokuja na uwekezaji wa mradi wa chuma na makaa
ya mawe Nchini.
1.
Kutakuwa
na wafanyakazi elfu kumi ambao wataajiriwa na kama kila familia itakuwa na watu
watatu watatu tu nyumbani basi tunaongelea ujio wa watu wapatao elfu thelathini
{30,000} watakaokuwa na mashikamano ya moja kwa moja na migodi na ajira. Hivyo
sisi tuwatizame wafanyakazi hao elfu kumi tu na baadhi ya mahitaji yao ya moja
kwa moja. Kama ifuatavyo:
-
Kila
mfanyakazi atahitaji maziwa lita moja kila siku, mayai mawili, na nusu kuku
kila siku. Bila kuangalia mahitaji mengine kwa jumla mahitaji yatakuwa kama
ifuatavyo:
i.
Kutakuwa
na mahitaji ya maziwa lita elfu kumi {10,000} kila siku
ii.
Kutahitajika
mayai elfu ishirini {20,000} kila siku
iii.
Kutakuwa
na mahitaji ya Nyama za kuku na kuku elfu tano {5,000} watakuwa wanahitajika
kila siku.
Hiyo ni sehemu ndogo tu ya fursa za
uwekezaji zitakazokuja una machimbo makubwa ya chuma na makaa yam awe. iMADS
imefanya tathmini Ludewa na kugundua kuwa hakuna kuku wa kienyeji wala wa
kisasa wa kutosha, na bei ya kuku mmoja inaanzia shilingi elfu 13 hadi elfu 20
kutegemea muuzaji na uzito wa kuku. Hakuna taxi hata moja, hakuna hotel za
kisasa, hakuna nyumba za kupangisha wala maeneo ya starehe.
Hadi iMADS inaondoka wilayani Ludewa,
kulikuwa na shamrashamra za kuweka sahihi mikataba baina ya wakandarasi na
TANROADS ya kukarabati na kupanua barabara ili kutengeneza kiwango cha
changarawe kwa dhumuni la kuwezesha vifaa vya wawekezaji vyenye uzito wa hadi
tani 150 na urefu wa hadi mita 15 ambavyo vitahitaji barabara ya aina yake
kuviwezesha vipite salama hadi migodini.
Makala hii itaendelea
ili kuonesha fursa zaidi zitakazokuja na uwezi wa migodi ya chuma na makaa yam
awe Ludewa.Moja ya mitambo inayosubiri ukarabati wa barabara ya Itoni hadi manda na Mkiu hadi Liganga |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni