Social Icons


Jumamosi, 17 Mei 2014

MASHINE YA KUKAMUA MAFUTA YA ALIZETI MKOMBOZI WA MTANZANIA


MASHINE YA KUKAMULIA MAFUTA YA ALIZETI

Mashine ya kukamua mafuta ya alizeti ni maja ya fursa nzuri za ujasiriamali Tanzania. Wakti baadhi ya nchi duniani zina uhaba mkubwa si wa ardhi tu, bali ardhi yenye rutuba, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani ambzzo  zimebahatika kuwa na ardhi kubwa yenya maeneo mengi yanayofaa kwa kilimo cha alizeti.

Mashine ya alizeti inayoonekaka katika picha hapo chini, ni mashine ndogo tu ambayo inaweza kumilikiwa na mtanzania yoyote lakini ina manufaa mtambuka kwa watanzania wengi kwa sababu zifuatazo: -

-                Mashine hiyo ni ndogo na inauzwa chini ya shilingi milioni kumi {10,000,000/=}

-                Mashine hiyo ina uwezo wa kukamua alizeti tani saba kwa siku

-                Mashine hiyo ina uwezo wa kukamua alizeti iliyolimwa kutoka wastani wa eka nne wa shamba lililolimwa bila utaalam na kwa muda wa siku mmoja.

-                Kwa maana hiyo mashine hiyo inahitaji tani {7 x 25  = 175 x 12 = 1,200} mia moja na sabini na tano kwa mwezi au siku 25 na itahitaji tani 1,200 kwa mwaka kama itaendeshwa kibiashara.

-                Mashine hiyo ndogo itahitaji zilimwe eka {4 x 25 x 12 = 1200} kwa mwaka ili iweze kufanya kazi kibiashara kwa mwaka mzima

Kwa taarifa za kibiashara, mchanganuo au andiko la mradi la mashine hiyo kwa mwekezaji yoyote mtarajiwa ni vizuri akawasiliana na iMADS kwa mawasiliano yaliyowekwa hapo chini ili kuwaza kufahamu mambo ya mengine ya msingi kibiashara. Inashauriwa kufahamu kwa mfano, tani saba za alizeti zatatoa mafuta kiasi gani, mashudu kiasi gani na kwa mwaka gharama za uendeshaji zikijumuisha mishahaara, gharama za umeme, bei za mafuta na mashudu pamoja na kufahamu aina na ukubwa wa maghala ya kuhifadhia alizeti ya kutosha mwaka mzima yanakuwa vipi.

Pia iMADS itatoa taarifa za gharama za kulima ekari 1,200 kiasi cha alizeti kitakachopatikana,  kiasi cha mafuta kitakachopatikana pamoja na bei zote zikijumuisha bei za mashudu.

Mkulima yoyote atakayelima kwa kufuata misingi ya utaalam atafanikiwa tu kwani kiasi cha mafuta nchini kinachozalishwa na watanzania kinatosholeza Taifa kwa kiasi cha asilimia 40 tu na asilimia 60 ya mafuta ya kula yananunuliwa kutoka nje ya nchi.

Uwekezaji wa kitaalamu katika eneo hili una tija nasi tupo tayari kushirikiana ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo, utaalam, wataalam wasimamizi wa mradi kama watahitajika na kusaidia upatikanaji wa mashine hizo.



Wasiliana nasi kupitia: -
Simu ya Kiganjani +255 767 111173/+255 773 111163


Maoni 10 :

  1. Hio picha mbona haionekani?

    JibuFuta
    Majibu
    1. Labda aina ya simu au laptop yako. Kwingine inaonekana

      Futa
  2. Hio 10million nikwa machine zote mbili ya kukamua na kusafisha? au kila moja na bei yake

    JibuFuta
  3. nimewfurahia.Nawezaje pata mashine hiyo mimi kama mjasiliamali?Napatikana Mugumu-serengeti.

    JibuFuta
  4. nimewfurahia.Nawezaje pata mashine hiyo mimi kama mjasiliamali?Napatikana Mugumu-serengeti.

    JibuFuta
  5. Mbona mashine sijaiona???

    JibuFuta
  6. Hiyo mashine uliyo iyelezea ipo kwa chino? Mbona haiyonekani!? Au tutumie rich...

    JibuFuta
  7. Naweza kuona inavyo fung'wa

    JibuFuta

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates