Social Icons


Jumatatu, 7 Aprili 2014

KILIMO CHA UFUTA {Sesame Farming in Tanzania}




Shamba la Ufuta
Ufuta baada ya Kuvunwa
Mafuta ya ufuta bei shs 6000/= kwa lita mwaka 2014
Kwa wajasiriamali wengi wanafahamu kuwa, ufuta ni zao linalotoa mafuta yenye thamani kubwa. Pamoja na matumizi ya kupikia, mafuta ya ufuta yanatumika katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumika kwa wanamichezo na wagonjwa kwa kuchulia misuli. Mafuta ya ufuta hayana aina mbaya ya mafuta na hivyo kuna namna yanatumika katika kupunguza pressure na maradhi yatokanayo na magonjwa ya moyo.

Ufuta unalimwa na kuandaliwa shambani kama ifuatavyo: -

1. Kilo moja ya ufuta ina mbegu zinazofikia 15,000
2. Kilo moja ya ufuta inatosha kupandwa katika eneo la eka moja
3. Katika eneo la futi moja shambani, hupandwa miche minne hadi nane
4. Mistari ya ufuta uliopandwa huwa umbali wa inch 15 had 36 kutegemea aina ya upandaji na ufuta wenyewe.
5. Mavuno ya ufuta kwa kiwango cha chini huwa ni kilo 360.
6. Mauzo ya mafuta ya ufuta hufikia shilingi 6,000/= kwa lita moja

Huwa hakuna tatizo la soko la ufuta Tanzania kwani, mafuta yote ya kula yanayotengenezwa Nchini yanatosheleza kwa asilimia 40 na asilimia karibu 60 ya mafuta ya kula huagizwa kutoka nje ya Tanzania.

Kwa Taarifa zaidi wasiliana na {i'MADS} Institute of Management and Development Studies Iringa. The former Sophist Tanzania College.





 

Maoni 10 :

  1. Elezea pia aina na bei ya pembejeo na gharama kwa ekari. Pia bei ya ufuta hadi na maangalizo muhimu. Ukiweza, onyesha anuani za Service providers muhimu. Kama kuna success story ya Mkulima Mdogo, iweke..

    JibuFuta
  2. Nataka kulima ufuta mvomero morogoro. Kabla sijaanza kulima nataka nikutane na wazoefu wa kilimo hiki 0753040819

    JibuFuta
  3. Kumbe hii blog ni yako mwalimu wangu Dominic Haule. Tulikutana Kilimanjaro. Nina mawasiliano yako. Nitakutafuta kaka

    JibuFuta
  4. kilomoja ndani ya heka moja au sijaelewa

    JibuFuta
  5. Nahitaji kulima ufuta naomba elimu ya kilimo nipo mtwara 0713020317

    JibuFuta
  6. Habari ndg zangu,
    Nina ekari 50 za ardhi inayopakana na mto wami unaotiririsha maji mwaka mzima. Shamba lipo wilaya ya Kilosa, kata ya Rudewa na shamba(pori) lipo katika kijiji cha Unone km 20 toka barabara ya lami ya Dumila Kilosa. kwa genuine buyer naomba tuwasiliani kwa 0653746459 au 0757614278 Bujaga Kadago Morogoro. Asanteni na karibuni.

    JibuFuta
    Majibu
    1. Sosthenes Christopher
      Habari ndugu,
      Haya mashamba bado yapo au yalishauzwa na kama yapo unayauza kwa bei gani kwa ekari moja?

      Futa
  7. Naomba kujua mbegu inayofaa kulimwa ya ufuta

    JibuFuta
  8. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  9. Naomba kujua mahali ambapo kuna kiwanda cha kukamua mafuta ya ufuta yenye kiwango kizuri na yanauzwaje kwa lita 1, 5 na 20?
    Ikiwa kuna anayetambua anijulishe hapa kwa kunipa majina ya kampuni au mtu mwenye hicho kiwanda na mawasiliano yake.

    JibuFuta

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates