Mkuu wa Kitengo cha Ujasiriamali cha {i'MADS} ndugu Dominick Haule, amekuwa akiendesha mafunzo ya Ujasiriamali kwa wanachama wa Posta na Simu SACCOS. Mafunzo ya Ujasiriamali ya Wanachama wa posta na simu Saccos yameandaliwa maalum kuzingatia awamu tatu ambazo zinajumuisha mambo yafuatayo: -
i. Ujasiriamali katika hatua ya utangulizi. Hapa maana ya ujasirimali, sifa na tabia za mjasiriamali, changamoto za ujasiriamali na jinsi ya kutambua aina ya fursa au biashara ya kuianzisha huzingatiwa.
ii. Awamu ya Pili huzingatia Fursa za Biashara. Hapa hatua zote au mchakato wa kuanza biashara hadi jinsi biashara inavyoweza kuwa imara na shamirivu hufundishwa. Kila mshiriki anahamasishwa kuchagua biashara katika hatua hii.
iii. Awamu ya tatu inazingatia uwezeshaji. Katika hatua hii andiko la mradi na jinsi ya kuandaa mchanganuo huzingatiwa.
Lengo ni kuwahamasisha wanachama wote wa Posta na Simu SACCOS kuanzisha miradi ya kiuchumi, Kuwaunganisha na masoko, kuwaunganisha na taasisi za fedha pamoja na kuwaunganisha na wauzaji wa malighafi na wauzaji wa technolojia mbali mbali.
Mafunzo ya ujasiriamali kwa Posta na Simu SACCOS Hufanyika nchi nzima au mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni