Social Icons


Alhamisi, 2 Januari 2014

Mhe. MBUNGE FILIKUNJOMBE, MANDA LUDEWA

Mheshimiwa Deo Filikunjombe amewataka wakazi wa Wilaya ya Ludwa kujipanga ili kuanza shughuli za Ujasiriamali kwa maendeleo yao binafsi, maendeleo ya familia zao, maendeleo ya Wilaya ya Ludewa na Maendeleo ya Tanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Filikunjombe aliyasema hayo wakati akiongea na waumini wa kanisa la Anglikana, Ilela Manda. Mbunge huyo machachari alisema, shughuli za ujenzi wa majengo mbali mbali yatakayokuwa miongoni mwa majengo ya mradi wa uwekezaji wa Miradi ya Machimbo ya Chuma na Makaa utaanza mwezi wa pili mwaka huu.

Pamoja na Mambo mengine, Mhe. Filikunjombe alisema, serikali imo katika maandalizi ya kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika kata ya Ilela, pembezoni mwa mto Ruhuhu. Baadhi ya picha za ziara ya Mhe. Deo Filikunjombe zipo hapa chini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates