Hatimae
Ndondondo si chururu Ludewa.
Kwa
kumbu kumbu zangu, Mheshimiwa Deo Filikunjombe Alikuja na vipau mbele viwili.
Vipaumbele hivi vimemfanya mbunge huyu machachari kutamka bungeni maneno ambayo
yamekuwa ni msingi wa mabadiliko wa mwenendo wa bunge letu na matokeo yake
yatawafikiwa watanzania wengi ikiwa ni pamoja na wajasiriamali wa Ludewa ambao
watashuhudia neema.
Neema
hii itawapata wale tu ambao si walalamishi, wabishi na watu ambao hawaishi
kuilaumi serikali kwa mambo mengi. Watakaofanya kazi watashuhudia mambo
yafuatayo: -
1. Watapata fedha nyingi kutokana na kilimo, uvuvi
na biashara kwani itakuwa ni gharama ndogo sana kusafirisha mzigo kutoka
Mikoani hadi Ludewa na Ludewa hadi mikoani.
2.
Nauli za mabasi na gharama za kusafirisha mizigo
zitashuka sana.
3.
Mzunguko wa fedha utaongezeka kwani Ludewa
imekaa sehemu nyeti kuliko Songea na Mbinga, kwani umbali toka dar ni mdogo
kulinganisha na maeneo hayo.
4.
Itakuwa ni rahisi sana kwa wadau waliooa Ludewa
na Walioolewa Ludewa kurudi home kuwekeza pamoja na kwamba watarudi kuwekeza
katika wakati mgumu kwani wajanja wanachukua maeneo kwa mamia ya maekari.
5.
Wafanya kazi elfu kumi wa migodi watafurahia
usafiri mzuri wa lami kutoka manda hadi Ludewa.
6.
Aliyelala Usimwamshe kwani utalala wewe. Ludewa
ni wilaya ndogo hivyo fursa hazitakuwa na muda mrefu zikiwa zimelala.
Habari
katika picha zina maelezo ya kina.
Ki
msingi wajasiriamali wa wilaya ya Ludewa na mikoa ya jirani, ni lazima
tumshukuru Mungu na tujitahidi kutoziacha fursa ambazo zitakwisha baada ya muda
mfupi kwani watu wenye upeo wameanza kuitazama na kuwekeza Ludewa kutoka pande
zote Tanzania.
Imekuwa
ni bahati kwani, hata katika Uchaguzi wa Nijeria, Wakati GoodLuck akiwa makamu
wa Rais, baadhi ya wananchi walisema, pamoja na kuwa huyu ni mpole badi, tumpe
tu urais kwani wakati mwingine nchi inaweza kuwa nzuri kwa kuongozwa na mtu
mwenye jina zuri tu. Hata kwa Ludewa, Kwa mujibu wa maelezo ya Mhe. Kolimba
Mwenyekiti wa CCM Wilaya aliweza sema kuwa, kila enzi ina wakati na mtu wake.
Ki ukweli Mhe wa Mbunge wa Ludewa ana bahati.
Fikiria
jinsi ukarabati wa barabara ulivyotakiwa uende haraka hadi km chini ya 250
kupewa wakandarasi wanne na wametakiwa kuimaliza ndani ya miezi miwili. Raha
zaidi ilikuwa pale ambapo sherehe za kuweka sahihi mkataba wa kufanya
matengenezo maalum kwa kiwango cha changarawe barabara ya kutoka Itoni Njombe
kupitia Ludewa hadi Mchuchuma na Nyingine ya kuanzia Mkiu hadi Liganga zilikuwa
zimeanza kazi. Ni jambo la kufurahisa kuona mkandarasi makini Boimanda aliweka
seti nne za vifaa maeneo tafauti tofauti kati ya Itoni na Mkiu {seti moja ni
Grader, Excavator, na Roller Compactor} na vilianza kazi kabla ya kuweka sahihi
mkataba.
Maelezo
ya picha pamoja na mambo mengine yanaonesha ushuhuda wa watu mbali mbali wakati
wa kuweka sahihi mkataba huo.
Habari
ya furaha kwa wajasiriamali wa Ludewa inaongezeka ndani ya wiki mbili baada ya
kushuhudia upanuzi wa barabara kiwango cha lami, sasa wanapewa km 50 kwa
kiwango cha lami. Ikumbukwe, Tayari Ludewa mjini kuna ujenzi unaendelea wa Km
10 za barabara ya Lami Kuzunguka takribani mitaa yote ya Ludewa. Wajasiriamali
wa Ludewa Mungu awape nini. ANGALIA PICHA HAPO CHINI. Habari na Picha na
{I’MADS}
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni