Mbunge
wa Kibaha Mjini Ndugu Silvestre Francis Koka aliamsha hisia za wafanyakazi wa
Shirika la Elimu Kibaha, wengi wao wakiwa walimu kwa kutoa historia yake ya
maisha kwa jinsi alivyopambana na umasikini mkubwa hadi kufikia kuwa na uwezo
mkubwa wa ki biashara alionao sasahivi.
Mheshimiwa
huyo, aliyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo yaliyofanywa na Taasisi ya
Decision Foundation DFL, Yenye makao yake makuu Iringa mjini na yaliyoongozwa
na katibu mtendaji wa Taasisi hiyo ndugu Dominic FN Haule.
Akisimulia
jinsi familia yake ilivyokuwa masikini, alisema yeye pia ni motto wa mwisho na
wa kiume pekee ambaye ameweza kufanya kila jitihada ya kuthubutu kutafuta
mawazo ya biashara, na kukumbatia kila fursa iliyokatiza mbale yake na alianza
na kuomba kazi ya umeneja wa Mgahawa wa Jeshi la kujenga taifa ambako alikwenda
kwa mujibu wa Sheria.
Kazi
hiyo ilimpatia hali ya kujiamini ambayo ilipelekea kuja kuomba na kufanikiwa
kupata tenda ya kuendesha mgahawa wa kampuni ya mabasi ya Taifa ya wakati huo
iliyokuwa ikiitwa KAMATA. Aliipata kazi hiyo kwa songo mbinde sana kwani
aliweza kufukuzwa ofisini humo zaidi ya mara tatu kwa kuwa mhusika aliyeombwa
amruhusu kuingia kwa meneja alisema wao walikuwa ni watoto na hawakustahili
hata kuthubutu kuomba kazi hiyo kwani kwa hakika wasingeliweza.
Baada
ya jitihada za muda, Mheshimiwa Koka alisema, alilazimika kwenda nyumbani kwa
Meneja wa kampuni hiyo ambayo haipo tena, na alifanikiwa kumuona meneja ambaye
aliwapatia kazi hiyo kwa masharti magumu yaliyojumuisha kuwa na mdhamini amaye
atakuwa tayari kulipa fidia ya uharibufu au uvunjifu wa mkataba huo kwani bado
naye aliwana vijana hao ambao walikuwa watatu kuwa bado ni watoto wadogo
waliokuwa wamemaliza kidato cha sita wakati huo na kuhudhuria JKT tu bila
uzoefu wowote.
Mheshimiwa
Koka alisema, baada ya kufanya kazi hiyo vizuri, ilipelekea yeye kuomba tena
kazi ya kulisha wafanyakazi katika viwanda vya TBL kazi ambayo aliweza kuifanya
kwa ufanisi na matokeo yake amefanikiwa kupata kazi zingine migodini.
Akielezea
tofauti yake na baadhi ya watanzania ambao hawajafanikiwa kiujasiriamali pamoja
na jitihada kubwa Mheshimiwa Koka alisema, yeye alikuwa tangu mwanzo ni mtu wa
kufuatilia kazi bila kukuta tama, anajali sana ubora wa bidhaa na huwa hakubali
kushindwa hata na makampuni ya kimataifa. Pamoja na hayo Mbunge huyo walisema,
ili mjasiriamali afanikiwe ni lazima aipende serikali na kuweza kwenda sambamba
na serikali kwani hata katika nchi za wenzetu, wajasiriamali wanaofanikiwa
kirahisi ni wale wanaozipenda serikali zao, wanaofuata sharia, taratibu na
kanuni na mwishowe huishia kwa serikali kuwanyanyua wafanyabiashara wa aina
hiyo kutokana na mafanikio yao.
Mheshimiwa
koka alitaja mapato yake ya jumla kwa mwezi ambayo ni makubwa sana japo bado
hajaridhika kwani anataka kuongeza kiasi cha mapato hayo pamoja na kuwa
ameajiri wafanyakazi wa kitanzania wapatao elfu mbili {2000} ambao anawalipia
kodi, akiba ya uzeeni na masurufu mengine wakiwemu na waajiriwa wazungu kumi na
moja {11}.
Mheshimiwa
Koka alisisitiza na kuwaomba watanzania wengine waanze kuiga mfano wake kwa
kutojali kuagiza na kuingiza technolojia kutoa nje ikizingatiwa kuwa dunia ya
leo ni ya utandawazi na sote tunalazimika kuwa wafanyabiashira wa kimataifa.
Habari
zingine za undani zitaandikwa wiki lijalo baada ya mahojiano yenye lengo ya
kuwahamasisha wajariamali wa kitanzania kuhusu jinsi ya kufanya vizuri katika
harakati za ukombozi binafsi wa ki uchumi.
+255
767 11 1173
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni