Mkurugenzi wa shirika la Elimu Kibaha Ndugu, Silipian Mtemba amesema atafanya kila jitihada ili wafanyakazi wote wa shirika hilo ambao idadi yao ni zaidi ya mia tisa (900) wapate elimu ya Ujasiriamali kwa awamu zote tatu zinazotolewa na taasisi ya Decistion Foundation iliyo na makao makuu yao iringa Tanzania.
Mkurugenzi huyo wa shirika hilo kongwa, aliyasema hayo wakati akihuduria mafunzo ya ujasiriamali ya siku mbili yaliyoanza tarehe 24 na kuishia tarehe 25 ya Mwezi huu wa Tano mwaka 2014 iliyokuwa ikiongozwa na Ndugu Dominick FN Haule katibu mtendaji wa Taasisi hiyo. Bwana Dominick FN Haule ni muasisi na mmoja ya wamiliki pia wa chuo cha uongozi na stadi za maendeleo cha Iringa {Institute of Management & Development Studies – Iringa {i’MADS}.
Semina hiyo ambayo ilianza na walimu 150 wafanyakazi wa shirika hilo na washiriki waalikwa wengine, ilihusu jinsi ya kuanza mchakato wa kuanzisha biashara, kumiliki biashara, jinsi ya kuziona fursa za biashara ambazo washiriki hao huwa wanapishana nazo kila siku na namna ya kufanya kazi na masoko, wataalam wa biashara na jinsi ya kutumia kwa busara mikopo.
Wakufunzi wa Mafunzo hayo walikuwa ni pamoja na Mmoja ya wakurungenzi wa DFL Ndugu, Shaali Ally Shaali, Ndugu Charles Musula na Ndugu Lukas Mahundi.
Historia fupi ya Shirika la Elimu Kibaha ambalo lilianzishwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerer mnamo mwaka 1970, lina maudhui yanayofanana moja kwa moja na dhana ya Ujasiria mali kwani kuanzishwa kwake kulilenga kutimiza ndoto ya mwalimu Nyerere ya Kuyakabili na kuyashambulia kwa wakati mmoja na sehemu moja maadui watatu wa Taifa yaani UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI.
Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya shirika hilo kuwa na madhumuni na malengo rasmi ya kupiga vita maadui wakubwa watatu wa maendeleo ya Taifa kuanzia siku ya kwanza ya Uhuru katika mwaka 1961.
Kuanza kwa Taasisi hiyo kulipata kufungwa mkono kwa kiasi kikubwa na kufadhiliwa kwa ushirikiano wa nchi za Dernmark, Sweeden, Finland na Norway.
Shirika hilo lina miradi ya elimu likimiliki shule, miradi ya maendeleo kama vile ufugaji na mradi wa afya wa Hospitali ya rufaa ya Tumbi iliyopo Kibaha. Habari hii fupi imeandikwa na Dominick. Kwa hisani ya {i’MADS
Casinos Near Casinos Near Casinos - Mapyro
JibuFutaFind your nearest 성남 출장샵 Casinos & hotels near Casinos in 군포 출장샵 North 경상북도 출장샵 America with Mapyro. 성남 출장마사지 Search for casinos 군포 출장마사지 and other gaming options near you.