Mwandishi
wa makala haya amebahatika kupata baadhi ya taarifa nyingi za uchimbaji na
wachimbaji wadogo ambao baadhi yao huamini kuwa kuna sehemu ya ushirikina
inatumika jambo ambalo wataalam wanalipinga vikali. Wachimbaji wadogo wa
dhahabu ambao nchini idadi yao inakaribia milioni tatu 3,000,000 wamekuwa na
changamoto kubwa tatu: -
i.
Tatizo la Kujaa maji migodi yao (mashapo au
shafts}
ii.
Tatizo la Mwamba mgumu wanaoukabili ndani ya
mgodi na jinsi ya kuutoa baada ya kuuvuja
iii.
Tatizo la mtaji
Wakati
utatuzi wa tatizo au changamoto ya kwanza ni kuitatua kwa kupata pampu za maji
zenye uwezo wa kutoa maji haraka wakati uchimbaji unaendelea, tatizo la pili la
mwamba linatatuliwa na mashine za kisasa za kupasulia miamba {jack hammers na
compressors} ambavyo vyote vinahitaji uwekezaji mkubwa kuzidi uwezo wao. Tatizo
la kutoa mwamba au vipande vya mawe na udongo wenye dhahabu linatatuliwa kwa
kupata mshine ya kunyanyulia mizigo aina ya {crane} zinye uwezo wa tani moja na
kuendelea kwani kwa kutumia ndoo, inawachukua matumizi ya nguvu nyingi na muda
mrefu sana. Mashine zingeliwawezesha kutoa kiasi kikubwa cha udongo na mawe kwa
muda mfupi na kufanya kazi ya kusaga kwa muda mrafu wakiwa namali ghafi nyingi
katika stoo zao.
Kuna
faida kubwa pia katika uchimbaji mdogo licha ya kuwa na changamoto mbali mbali
kwani kwa mchimbaji aliyejipanga anakuwa na uwezo wa kuzalisha hadi kilo moja
kila siku. Mwandishi wa makala haya alitembelea mgodi mmoja wa mchimbaji mdogo
ambaye uwezo wake ulikuwani nusu kilo ya dhababu kwa siku. Uwekezaji unaweza
kutumia kiasi cha shilingi milioni mia tatu 300,000,000/= kwa wachimbaji wadogo
wenye uwezo na wanaofuata utaalamu kwani maafisa madini wana taaluma nzuri ya
kushauri masuala ya uchimbaji na kumuwezesha mchimbaji mdogo kufikia uwezo huo.
Shilingi milioni mia tatu siyo nyingi ukilinganisha na kiasi cha dhahabu ya
nusu kilo kinachopatikana kila siku kwani kiasi hicho kinaweza kuuzwa hadi
shilingi milioni 40 {nusu kilo ya dhahabu.
Wito
ni kwa watanzania wanaotaka kuwekeza wawasiliane na iMADS ili wapate taarifa
kamili na maandiko ya miradi ya jinsi ya kuwekeza katika madini aina ya dhahabu
kwani kitengo hiki cha chuo, kina taarifa zote muhimu za kibiashara za
uchumbaji wa dhahabu.
Pamoja
na maraha ya faida, hiyo huwa ni kwa wawekezaji, lakini kwa upande wa
wachimbaji wadogo wana machungu yao kama yalivyoshudiwa na mwandishi wa makala
hayo alipotembelea migodi na kujikuta analazimika kusaidia kusimamia shughuli
za maafa na majanga katika baadhi ya maeneo. Picha hapo chini zinaonesha
wachimbaji wadogo ambao wengi wao hawajajipanga, hawafuati taratibu za usalama
na kujiweka muda mwingi hatarini. Wachimbaji waliangukiwa na mgodi, walikaa
ndani ya shimo kwa siku tatu na siku ya nne tulifanikiwa kuwatoa wakiwa hoi,
bila chakula siku nne, bila maji na hewa kiduchu mno. Walikuwa hawana nguvu na
hawakuamini kuwa waliokolowa. Wachimbaji hao wadogo walidai kuwa kama
tusingelikuwepo sisi wageni, basi ingelikuwa mwisho wao kwani baadhi ya
wachimbai walikuwa na imani potofu kuwa, eti mgodi wenye maafa hutoa dhahabu
nyingi {hutapika dhahabu} kitu ambacho siyo cha kweli, kwani wachimbaji wengi
wanaofanikiwa ni wale wanaowatumia wataalam ao maafisa wa madini waliobobea
katika taaluma zao.
Kwa
taarifa zaidi na maelezo au kama una mchango wa mawezo wasiliana na
Dominickhaule@gmail.com Cell Phone:
0767 11 1173
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni