Social Icons


Ijumaa, 20 Juni 2014

TAMU ZENYE CHUNGU KATIKA UCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU TANZANIA


HAKIKA KUNA TAMU ZENYE CHUNGU NA CHUNGU ZENYE SALAMA KWA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU TANZANIA
Sheria za madini nchini pamoja na mambo mengine, haziruhusu mtu kushika, kukutwa au kufanya biashara ya madini yoyote bila ya kuwa na leseni. Sheria hiyo inamruhusu mwekezaji yeyote wa ndani na nchinya nchi, kuomba leseni ya uchimbaji sehemu yeyote kwa mujibu wa sheria na kutoa fidia kwa mali zilizopo juu ya ardhi kwa wote watakaokuwepo katika eneo lililoombewa kibali. Ndiyo maana baadhi ya watanzania hawaielewi vizuri sheria hii itakayoelezewa vizuri hapo chini. Utaratibu huu wa kuchimba dhahabu kienyeji na kuiuza kienyeji ulimkumba mchimbani mmoja huko Nyalugusu, Mkoa wa Geita ambaye alifanikiwa kupata madebe matatu yaliyojaa dhahabu na kukataa fedha badala yake aliwaomba wanunuzi eti wampatie treni {gari moshi}.
Mzee huyo aliyejitamblisha kwa jina la mangida, alisema yeye shida yake ilikuwa apewe treni aimiliki kwani aliipenda sana. Watu walio karibu nae walimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa, wanunuzi hawakumwelewa muuzaji huyo na waliamua kumuacha hotelini mwanza na kuelekea huko India. Tukio hili ni la muda mrefu, takribani miaka 40 iliyopita. Picha chini ni Muuzaji huyo wa dhahabu akiwa na mwandishi wa makala hayo bwana Dominick Haule.
Kisheria, mzee huyu angeliweza kukamatwa na kushtakiwa kwa kisa la kukutwa na madini bila ya kuwa na leseni wala kibali. Huenda angelikuwa mchimbaji mwenye leseni, maafisa wa madini wangelimsaidia kuuza madini hayo.
Sheri za madini zina watatanisha sana baadhi ya watanzania hususani wale wenye mashamba yaliyopo maeneo yenye madini. Ukiwa na shamba na hata kama una hati ya kumiliki shamba hilo, sheria inaruhusu utoaji wa leseni shambani kwako ili mwekezaji anayetafuta mali iliyopo chini ya ardhi, aweze kuipata mali hiyo kwa sharti ya kukulipa fidia ya kilichopo juu ya ardhi kwani ardhi ni mali ya serikali. Ni vizuri watanzania wakachukua hatua ya kuzifahamu baadhiya sheria za madini ili waweze nao kuomba leseni za madini kama watahitaji kufanya hivyo badala ya kuishia kulia na kulalamika sana kitu ambacho hakitamsaidia mtanzania wala Taifa kwa ujumla.

Kwa taarifa zaidi, maoni au maswali wasiliana na dominickhaule@gmail.com
Simu: 0767 11 1173.

Bwana Dominick FN Haule {katikati} akimhurumia mzee Mangida {kulia kwake} kwa kupoteza madebe matatu ya dhahabu
Mwandishi wa Makala haya {katikati} akizungumza na mzee Mangida {aliyekaa kushoto} ambae alikataa fedha ili auze dhababu madebe 3 kwa kupewa Trani {Gari moshi}

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 

IMADS

INSTITUTE OF MANAGEMENT AND DEVELOPMENT
STUDIES- IRINGA

Sample Text

Sample Text

 
Blogger Templates